MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto ameitaka Serikali kutoipatia 
leseni ya uchimbaji wa madini ya urani, kampuni ya Uhuru One hadi iilipe
 Serikali kodi ya Sh297 bilioni.
Zitto ambaye pia ni Naibu 
Kiongozi wa Upinzani Bungeni, alitoa pendekezo hilo bungeni mjini Dodoma
 jana aliposimama na kutumia kanuni ya 68(1) kueleza kutoridhishwa na 
majibu ya Serikali kwenye swali la 353.
Katika swali hilo, Mbunge
 wa Jimbo la Mkoani, Ali Khamis Seif (CUF), alitaka kufahamu Serikali 
itanufaika vipi na uchimbaji wa urani utakaoanza mwakani katika hifadhi 
ya Selous.
Katika majibu yake, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alisema uchimbaji wa madini hayo utailipa Serikali
mrabaha wa asilimia tano ya urani yote itakayozalishwa.
Pia
 alisema Serikali itashiriki katika miradi ya urani kwa kuwa na hisa 
bila kuwekeza mtaji wowote na kupata gawio kama mwana hisa,
achilia mbali kodi mbalimbali itakazolipwa.
Hata
 hivyo, Zitto alisema baada ya Kampuni ya Mantra ya Australia 
kukamilisha kazi ya utafiti wa urani, iliuzwa kwa kampuni ya Urusi
inayojulikana kama ARZM kwa Dola za Marekani 980 milioni.
Alisema
 baada ya mauzo hayo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) , walitaka 
walipwe asilimia 20 kama kodi ambayo ni Dola 186 milioni za Marekani, 
sawa na Sh297 bilioni.
“Uhuru One inayotaka kuchimba madini hayo 
ya Urani ni kampuni tanzu ya ARZM ya Urusi tutasikitika sana kama leseni
 ya uchimbaji itatolewa kabla ya kulipwa kwa kodi hiyo,” alisema.
Hata
 hivyo, katika maelezo yake hayo, Zitto hakufafanua sababu za fedha hizo
 kutolipwa hadi sasa lakini alisisitiza kuwa ni vyema
Serikali isitoe leseni ya uchimbaji hadi zilipwe.
Akijibu
 hoja hiyo, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo 
alisema, Serikali inafahamu zaidi kuhusu jambo hilo na kwamba
leseni haijatolewa na haitatolewa.
 
No comments:
Post a Comment