Ukosefu wa nguvu za kiume nchini twaweza kusema  ni janga. Hii 
ni kutokana na tafiti zilizowahi kufanywa na pia kuzagaa kwa vibao vya 
matangazo kuhusu dawa au tiba ya tatizo hilo.
Tatizo hili halipo kwa wazee kama ilivyodhaniwa zamani, bali hata kwa vijana, wake kwa waume wamekuwa wakiguswa na tatizo hilo.
Sababu nyingi zimewahi kuanishwa kuchochea ugumba 
kwa wanaume ikiwamo maradhi, kutazama luninga kwa muda mrefu na 
kutofanya mazoezi.
Hivi karibuni wataalamu katika Jarida la Jinsia na
 Tiba  la nchini Uingereza, lililochapishwa Januari lilieleza sababu kuu
 duniani zinazochochea ugumba kwa wanaume iwe wa muda mrefu au wa 
kudumu.
Taasisi ya Taifa ya Afya ya nchini Marekani (NIH) 
inaeleza kwamba sababu za jumla za ugumba ni umri na  asilimia nne ya 
wanaume wenye umri wa miaka 50  na kuendelea wanaweza kuwa na tatizo 
hilo wakati nusu ya wanaume wenye umri wa miaka 75 wanakumbwa na ugumba.
Daktari wa Upasuaji na Nguvu za Kiume katika Chuo 
Kikuu cha Tiba cha Maryland,  Dk Andrew Kramer anasema karibu nusu ya 
wanawake na wanaume wote duniani wanakosa nguvu za kiume aidha moja kwa 
moja au katika nyakati fulani za maisha yao.
Madereva 
Dk Kava anasema wakati wa zama za chuma ilibainika
 kwamba wanaume wanaoendesha baiskeli kwa muda mrefu, waendesha farasi 
na madereva wa magari kwa muda mrefu wamo hatarini kukosa nguvu za 
kiume.
Jarida la tiba lilifanya utafiti na kubaini kuwa 
asilimia nne ya wanaume wanaoendesha baiskeli kwa saa tatu au zaidi kwa 
wiki wanapata matatizo ya nguvu za kiume.
Anasema unapokaa kwenye gari, farasi au baiskeli 
kwa muda mmrefu unaweka nguvu katika neva na mishipa midogo inayobeba 
damu kwenda katika uume.
Anafafanua kwamba uendeshaji wa vyombo hivyo kwa muda mrefu unaharibu mishipa midogo na damu haiendi inavyotakiwa katika uume.
CHANZO: GAZETI MWANANCHI
CHANZO: GAZETI MWANANCHI
 
No comments:
Post a Comment