CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimewatahadhalisha
Wanawake watakaobakwa kutooga au kubadilisha nguo kwa sababu kufanya
hivyo kunapoteza ushahidi wa kumtia hatiani Mtuhumiwa.
Taarifa
iliyoandaliwa na Tamwa kupitia Mtandao wake wa kijamii zinasema,
Madaktari nchini wameshauri wanaobakwa kufika haraka kituo cha polisi
kuchukua PF3 na kuipeleka hospitali kwaajili ya kupata matibabu ikiwamo
dawa za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Akinuliwa na
Chama hicho, Dk Zuberi Mzige wa hospitali ya Mwananyamala iliyopo jijini
Dar es S alaam alisema , kumekuwa na tabia ya watoto wa kike
wanaofikishwa hospitalini baada ya kubakwa kutokuwa na ushahidi kutokana
na kuoga au kubadilisha nguo.
“Wengine wanafikishwa hospitalini
wakiwa wamecheleweshwa hivyo kuwa kwenye hatari ya maambukizo ya HIV”
taarifa ilimnukuu.Naye Dk Prisca Berege anayeshughulikia magonjwa ya
watoto katika hospitali ya Mwananyama alisema , mji wa Dar es Salaam una
tatizo la ubakaji hasa kwa watoto.
Alizungumza hayo na
Wanahabari walioshiriki katika mkutano wa utafiti wa maswala ya ukatili
wa kijinsia ulioandaliwa na TAMWA hivi karibuni katika Manispaa ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
“Kila siku hospitali ya Mwananyama lazima tupokee watu watatu waliobakwa ambao ni wanawake na watoto” alisema Dk Barege.
Dk
Barege aliwashauri wazazi kuepuka kuwatuma watoto wao nyakati za usiku
na kuwatahadharisha watoto wa kike kuwa makini na uhusiano baina yao na
wanaume waliozoeana.
Alitoa mfano wa binti mmoja ambaye hivi
karibuni alibakwa mchana na mwanaume aliyemwamini kama kaka n amwajiri
wake baada ya kumwita nyumba ni kwake ili wapange kazi ya kufanya.
No comments:
Post a Comment