Wednesday, June 20, 2012

UGANDA KUZIFUNGIA TAASISI ZINAZOSHABIKIA NDOA ZA JINSIA MOJA


Waziri wa maadili nchini Uganda   Simon Lokodo  amesema atayafunga mashirika 38  yasiyo ya kiserikali (NGO's) zinazoshabikia ndoa za jinsia moja(homosexuality ) nchini humo.

Waziri huyo anasema

"Nimechunguza na kujiridhisha bila kuwa na mashaka yoyote kuwa haya mashirika yamekuwa yakuhusika kuchochea, kuhimiza  na kutayarisha watu  watakaoingia katika  ndoa za jinsia moja”

Licha ya kutozitaja kwa majina taasisi hizo , waziri Lokodo amesema ameshawasilisha majina ya taasisi hizo kwa wizara ya mambo ya ndani ambapo itayafunga na hawatakuwa na haki ya kikatiba kuchochea vitendo hivyo nchini Uganda.


Muswada wa adhabu ya kifo kwa wanaojihusisha na vitendo vya ndoa za jinsia moja uliwasilishwa katika Bunge la nchi hiyo toka mwaka 2009

No comments:

Post a Comment