Kwa bahati mbaya sana katika maisha yangu sikupata nafasi ya kujua upendo wa wazazi kutokana na kutokuwa nao katika wakati ambao nilidhani niliwahitaji sana, namshukuru Mungu amenipa watu wanaonipenda kama mtoto wao wa kuzaa, wananisaidia na wamekuwa wakinielekeza kufanya yaliyo mema.
Siwezi kutaja mafanikio yangu bila kuwataja kaka na dada zangu lakini pia mawifi na mashemeji zangu, wamenivumilia toka nikiwa mtoto nisiyeelewa nini maana ya maisha hadi leo nimeweza kujisimamia mwenyewe.
Katika mengi pia namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuiishi ndoto yangu, tangu nikiwa mtoto nilitamani sana kuwa mwandishi wa habari na mtangazaji, japo sikujua ntapitia mlango gani kulifanikisha hilo. Leo napoandika haya mimi ni mwandishi wa habari kwa muda wa miaka miwili sasa na amenipa neema kubwa na kibali cha kufanya kazi yangu hata nje ya mipaka ya nchi yangu.
Nikiwa katika moja ya maandalizi ya kipindi cha television |
Nikiwa katika maandalizi ya kutengeneza kipindi changu cha kwanza kabisa Kigoma |
Najua kuna makuu yaliyoko mbele yangu maana hata sasa bado sijafika mahali ambapo Mungu amenikusudia, Najua kwa neema na kwa wakati wake nitafika na ataniwezesha kufanya yote.
Kwangu kikubwa ni matumaini katika Mungu maana hana asiloliweza katika katika maisha yetu. When the whole world turns against me i know where i can find hope.
Nawashukuru sana marafiki zangu, familia yangu na wafanyakazi wenzangu.
No comments:
Post a Comment