ROSE Kamili anayedai kuwa ni mke wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod
Slaa, amefungua kesi Mahakama Kuu akiiomba isimamishe ndoa ya kiongozi
huyo na mke mwingine inayotarajiwa kufungwa Julai 21, mwaka huu wilayani
Karatu Mkoa wa Manyara.Dk Slaa anatarajia kufunga ndoa na mchumba wake
wa siku nyingi, Josephine Mushumbusi.
Kamili ambaye ni Mbunge wa
Viti Maalumu (Chadema), pia anaiomba Mahakama iamuru Dk Slaa amlipe Sh50
milioni za fidia aliyotumia kujihudumia pasipo matunzo ya mumewe huyo.
Mbunge
huyo kupitia kwa Wakili wake, Joseph Thadayo, aniomba pia Mahakama
iamuru Mushumbusi amlipe kiasi cha Sh500 milioni za fidia ya maumivu
aliyoyapata kutokana na kitendo chake cha kuingilia ndoa yao.
Kesi hiyo namba nne ya mwaka 2012 iliyopangwa kusikilizwa na Jaji Lawrance Kaduli, inatarajiwa kutajwa kwa mara ya kwanza leo.
Katika
hati hiyo ya madai, mbunge huyo anadai kuwa ndoa inayotarajiwa kufungwa
kati ya Dk Slaa na Mushumbusi ni batili kwa sababu kuna ndoa nyingine
halali na inayoendelea kuishi kati ya Slaa na Kamili iliyofungwa mwaka
1985.
Alidai baada ya kufugwa kwa ndoa hiyo, Juni 18, 1987
walifanikiwa kupata mtoto wa kike anayeitwa Emiliana Muchu na baadaye
Septemba 23, 1988 walipata mtoto mwingine wa kiume, Linus Amsi.
Katika
uhusiano wao, Dk Slaa akiwa ni Padri wa Kanisa Katoliki, alifanya
taratibu zilizomwondosha katika nafasi hiyo na kuanza maisha ya familia.
Baada
ya taratibu hizo, jamii ya Watanzania iliwatambua kama mume na mke na
hata kumbukumbu za hati za kimataifa kama za kusafiria ziliwatambua kuwa
wanandoa.
Kamili aliendelea kudai katika maelezo hayo kuwa yeye
na Slaa waliishi maisha ya ndoa yenye amani yaliyowawezesha kupata mali
kadhaa walizomiliki kwa pamoja ikiwemo nyumba iliyopo kwenye Kiwanja
namba 609 Kitalu E iliyopo Sinza, Dar es Salaam, nyumba ya makazi
iliyopo Kijiji cha Gongali huko Karatu na vifaa mbalimbali vya nyumbani.
Hati
ya mashtaka imeendelea kudai kuwa uhusiano kati ya Slaa na Kamili,
ulianza kuharibika mwaka 2009, baada ya mume huyo kuwa na uhusiano na
mwanamke mwingine kinyume cha sheria… “Tangu mwaka huo 2009, Slaa
akaitelekeza familia yake kwa kutoipatia huduma,” imeeleza hati hiyo.
Kamili
anaiomba Mahakama iamuru kuwa yeye na Dk Slaa bado ni mke na mume na
kwamba Mushumbusi aliingilia ndoa yao hivyo izuie ndoa inayotajiwa
kufungwa Julai 21, mwaka huu huko Karatu, Manyara.
Kamili pia
amewasilisha hati hiyo ya mashtaka kwa Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo
akimweleza Askofu Mkuu huyo wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam kuwa moja
ya Parokia za Dar es Salaam zina taarifa ya ndoa hiyo.
Nakala ya
madai hayo pia imewasilishwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu, Msajili wa
Ndoa na kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbulu.
Dk Slaa: Nimeyazoea
Alipotakiwa kuzungumzia kesi hiyo nje ya Mahakama, Dk Slaa alisema: “Hayo mambo nimeyazoea na kimsingi hayanipi shida yoyote.”
Alipoulizwa
endapo anajipanga vipi kulipa fidia hiyo alijibu: “Kesi ni kesi hivyo
siyo kila kinachoombwa kwenye kesi lazima kilipwe.”
Hata hivyo, Dk
Slaa alisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa undani kwa kuwa liko
kwa mawakili wake lakini akasema amebaini kuwa hizo ni hila na michezo
michafu ya kisiasa.
“Kwanza siyo pingamizi moja tu, kuna pingamizi mbili mahakamani lakini kwa ufupi ifahamike kuwa hizo ni hila.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment