Ukosefu wa nguvu za kiume nchini twaweza kusema ni janga. Hii
ni kutokana na tafiti zilizowahi kufanywa na pia kuzagaa kwa vibao vya
matangazo kuhusu dawa au tiba ya tatizo hilo.
Tatizo hili halipo kwa wazee kama ilivyodhaniwa zamani, bali hata kwa vijana, wake kwa waume wamekuwa wakiguswa na tatizo hilo.
Sababu nyingi zimewahi kuanishwa kuchochea ugumba
kwa wanaume ikiwamo maradhi, kutazama luninga kwa muda mrefu na
kutofanya mazoezi.
Hivi karibuni wataalamu katika Jarida la Jinsia na
Tiba la nchini Uingereza, lililochapishwa Januari lilieleza sababu kuu
duniani zinazochochea ugumba kwa wanaume iwe wa muda mrefu au wa
kudumu.
Taasisi ya Taifa ya Afya ya nchini Marekani (NIH)
inaeleza kwamba sababu za jumla za ugumba ni umri na asilimia nne ya
wanaume wenye umri wa miaka 50 na kuendelea wanaweza kuwa na tatizo
hilo wakati nusu ya wanaume wenye umri wa miaka 75 wanakumbwa na ugumba.
Daktari wa Upasuaji na Nguvu za Kiume katika Chuo
Kikuu cha Tiba cha Maryland, Dk Andrew Kramer anasema karibu nusu ya
wanawake na wanaume wote duniani wanakosa nguvu za kiume aidha moja kwa
moja au katika nyakati fulani za maisha yao.
Madereva
Dk Kava anasema wakati wa zama za chuma ilibainika
kwamba wanaume wanaoendesha baiskeli kwa muda mrefu, waendesha farasi
na madereva wa magari kwa muda mrefu wamo hatarini kukosa nguvu za
kiume.
Jarida la tiba lilifanya utafiti na kubaini kuwa
asilimia nne ya wanaume wanaoendesha baiskeli kwa saa tatu au zaidi kwa
wiki wanapata matatizo ya nguvu za kiume.
Anasema unapokaa kwenye gari, farasi au baiskeli
kwa muda mmrefu unaweka nguvu katika neva na mishipa midogo inayobeba
damu kwenda katika uume.
Anafafanua kwamba uendeshaji wa vyombo hivyo kwa muda mrefu unaharibu mishipa midogo na damu haiendi inavyotakiwa katika uume.
CHANZO: GAZETI MWANANCHI
CHANZO: GAZETI MWANANCHI
No comments:
Post a Comment